“Forgive other people for many things, but do not forgive yourself anything.” —PUBLILIUS SYRUS
Kama kuna urahisi wowote unaoweza kuutoa kwenye maisha, basi wape watu wengine urahisi huo, ila usijipe wewe mwenyewe.
Wasamehe wengine kwa makosa wanayofanya, lakini usijisamehe mwenyewe mpaka pale umerekebisha ulichokosea.
Waruhusu wengine wajipe sababu ya kutokufanya walichopanga, lakini usijiruhusu kwa namna yoyote ile kujipa sababu ya kutofanya ulichopanga.
Wape wengine ruhusa ya kufanya kawaida, lakini usijiruhusu kwa namna yoyote ile kufanya kawaida.
Wasamehe wengine pale wanapojiwekea misingi na kutokuiishi, lakini usijisamehe wewe mwenyewe kwa kufanya hivyo, ishi misingi uliyojiwekea au jiadhibu pale unaposhindwa kuishi misingi hiyo.
Bila ya kujijengea nidhamu kali, ambayo wengine wanaona unajitesa, safari hii ya mafanikio itakuwa ngumu sana kwako.
Mafanikio siyo rahisi, lazima ujitoe kweli ili kuyafikia, na katika kujitoa huko, lazima uwe tayari kuumia.
Usiyakimbie maumivu.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania