A stone falls on a pot—woe to the pot; a pot falls on a stone—woe to the pot; in every case, it is bad for the pot. —The TALMUD
Jiwe likianguka kwenye chungu, ni chungu ndiyo kinavunjika.
Chungu kikianguka kwenye jiwe, bado ni chungu ndiyo kitakachovunjika.
Jiwe na chungu vinawakilisha njia mbili za kuyaishi maisha hako.
Unaweza kuwa kama chungu, ambapo kila kinachotokea kinakuathiri sana kwenye mipango uliyokuwa umejiwekea.
Au unaweza kuwa kama jiwe ambapo chochote kinachotokea hakiathiri mipango yako, unaendelea kama ulivyopanga, kinachotokea ndiyo kinaathirika chenyewe pale kinapokutana na wewe uliye imara.
Chagua kuwa kama jiwe, siyo kwa ugumu au ubishi, bali kwa msimamo na kutoyumbishwa na chochote.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania