“Live your life in such a way that you neither hide nor have a wish to display your life to people.” – Leo Tolstoy
Ishi maisha yako kwa namna ambayo huna chochote ambacho unahitaji kukificha ili wengine wasione au kujua na pia kuna chochote ambacho unataka sana kuonesha wengine waone au kujua.
Haya ni maeneo mawili ambapo wengi wanapoteza sana muda wao,
Kwa kufanya mambo fulani yasiyo sahihi na hivyo kuhitaji nguvu nyingi kuyaficha,
Au kuingia kwenye mashindano ya kuwa na vitu fulani ili wengine waone na wewe unacho.
Wewe ondoka kwenye hayo,
Fanya kile kilicho sahihi mara zote hivyo huna cha kuficha,
Sema ukweli mara zote hivyo huna cha kukumbuka ili usiumbuke,
Kuwa na kile ambacho ni muhimu kwako na unachokijali na siyo kile ambacho kila mtu anacho na unataka uwe nacho ili na wewe uonekane.
Fanya kilicho sahihi na ishi maisha yako, haya yatakupa utulivu mkubwa sana kwenye maisha.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania