“It is a big mistake to think that faith is immutable, that it does not change over generations. The longer mankind exists y its faith becomes simpler and stronger. And the simpler and stronger our faith becomes, the better we live.” – Leo Tolstoy
Ni makosa makubwa sana kufikiri kwamba imani ya mtu haipaswi kubadilika.
Imani hubadikika kati ya vizazi na ndani ya mtu mwenyewe.
Unapokuwa mdogo, unaamini kila kitu unachoaminishwa na wengine.
Ubalishwa kila aina ya imani na unapokea bila kuhoji au kujiuliza ni sahihi.
Ukiwa kijana na mtu mzima, una hatari ya kuwa na imani kali zaidi, imani isiyolegea au kubadilika.
Imani hiyo huwa ngumu pia na inakuwa vigumu kwako kuibadili.
Unapokuwa mtu mzima zaidi na mzee, unagundua kwamba sehemu kubwa ya imani ulizoishi nazo miaka yako mingi hazikuwa sahihi,
Lakini bado kuzibadili inakuwa vigumu kwako.
Kila unavyozidi kwenda, imani yako inapaswa kubadilika.
Na inapaswa kubadilika kuwa rahisi na imara,
Rahisi kwako kuielewa na kuielezea kwa wengine.
Imara ili kuweza kukupa kitu cha kusimamia.
Epuka sana itikadi kwenye imani yoyoye uliyonayo.
Epuka kujiona wewe ni bora au sahihi zaidi ya wengine.
Kuwa mnyenyekevu na tengeneza imani sahihi kwako na wengine pia.
Kuamini kwamba imani uliyonayo haipaswi kubadilika,
Ni sawa na kuamini hadithi za sungura na fisi ulizokuwa unaambiwa utotoni ni za kweli.
Imani yako ndiyo msingi mkuu wa maisha yako,
Hakikisha umeijenga na kuibadili ili iweze kuendana na wewe.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania