“Do not despair. Do not be disappointed if you see that you cannot accomplish all the good which you would like to accomplish. If you fall, try to stand up; try to overcome the obstacle before you. Get to the heart of the matter, to the essence of things.” —MARCUS AURELIUS
Maisha yangekuwa rahisi kama ambavyo wewe unataka yawe,
Kwamba uanzishe tu biashara na upate mafanikio haraka,
Uwekeze mahali na kuvuna faida tu,
Usichoshwe na kazi yoyote unayofanya,
Upate kila unachotaka.
Jamii ya binadamu ingeshapotea hapa duniani.
Ugumu wa maisha, changamoto mbalimbali tunazokutana nazo, ndizo zinazotufanya kuwa imara.
Ndizo zinatufanya kujisukuma zaidi, kufanya makubwa zaidi.
Hivyo usiombe mambo kuwa rahisi, bali kazana kuwa bora ili kuweza kupambana na kila linalotokea.
Kila kiumbe kwa asili yake kinapambana na magumu yake,
Na wewe pambana na magumu yako,
Kwa sababu hakuna aliyekuahidi mambo yatakuwa rahisi,
Na kama yupo basi alikudanganya.
Mambo ni magumu lakini yanawezekana.
Usione wengine wanacheka ukafikiri mambo ni rahisi kwao,
Usiangalie nyasi za upande wa pili ukasema ni za kijani kuliko zako,
Nyasi zozote zinaweza kuonekana za kijani ukiwa mbali.
Sogea karibu na utajionea wazi, siyo nyasi zote zina ukijani.
Na kama nyasi za mwenzako zina ukijani kuliko zako,
Ni kwa sababu amezinyeshea na kuzitunza vizuri,
Badala ya kutamani kuwa na nyasi zake, kwa nini usianze kunyeshea na kutunza zako vizuri?
Safari ya mafanikio uliyochagua itakuwa ngumu,
Utakutana na magumu na changamoto nyingi,
Usikate tamaa, kila mtu anapitia unayopitia, kwa nyakati na namna tofauti.
Ukianguka inuka tena, endelea na safari.
Vuka kila kikwazo unachokutana nacho.
Na kama huwezi kuvuka kikwazo, basi kitumie kikwazo hicho kuwa njia.
Usiogope, ndani yako kuna uwezo mkubwa,
Utaujua na kuweza kuutumia unapokutana na magumu.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania