“Nothing can make a person’s soul softer than the understanding of his own blame, and nothing can make one harder than the desire always to be right.” —After the TALMUD

Kama unataka kuwa sahihi kila wakati, maana yake haupo tayari kujifunza.
Hili linaufanya moyo wako kuwa mgumu, unakuwa na kiburi na hata majivuno, ukiamini unajua kila kitu.
Lakini hakuna mtu yeyote ambaye anajua kila kitu, ambaye hana kipya cha kujifunza.
Kwa kila mtu na kwa kila jambo, kuna unachoweza kujifunza.
Ukiwa tayari kuelewa na kukubali makosa yako,
Ukawa tayari kuona mapungufu yako,
Unaufanya moyo wako kuwa mwepesi, unakuwa mnyenyekevu na kuwa tayari kujifunza na kubadilika.
Kwa namna hii unaziona fursa nyingi za kuwa bora zaidi ya pale ulipo sasa.

Sisi binadamu ni kazi iliyopo kwenye matengenezo muda wote,
Hakuna siku tunaweza kujiambia tumeshakamilika,
Hivyo usijidanganye kwamba wewe ni mkamilifu, unajua kila kitu na huwezi kukosea.
Usitegemee hayo kwa wengine pia.
Jua unafanya makosa na wengine hivyo hivyo.
Muhimu ni kuyakubali makosa na kuyasahihisha huku ukijifunza kutokuyarudia.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania