“A huge amount of knowledge is accumulated at present. Soon our abilities will be too weak, and our lives too short, to study this knowledge. We have vast treasures of knowledge at our disposal but after we study them, we often do not use them at all. It would be better not to have this burden, this unnecessary knowledge, which we do not really need.” — IMMANUEL KANT

Tunaishi kwenye zama za taarifa,
Ambapo taarifa na maarifa vinapatikana kwa wingi mno.
Yaani ni kama tunaogelea kwenye bahari ya maarifa na taarifa.
Wengi katika hali hii, hutapatapa wakitaka kujua kila kinachoendelea.
Itakuchukua mamilioni ya miaka kama unataka kuangalia videzo zote zilizopo kwenye mtandao wa youtube.
Pia utahitaji mamilioni ya miaka kama utataka kusoma kila kitabu kilochowahi kuandikwa.
Kama una tv na king’amuzi nyumbani kwako, unajua uka stesheni zaidi ya 100 unazoweza kuangalia, na huwezi kuangalia zote kila siku.

Badala ya kukimbizana na kujua kila kitu, jambo ambalo huliwezi,
Unapaswa kujua unataka nini, kisha tafuta maarifa na taarifa zinazokusaidia kile unachotaka.
Ubaya ni kwamba hujui unachotaka, na hivyo unahangaika na kila maarifa na taarifa.

Hata walimu na washauri wako wengi mno,
Na wakati mwingine wanayofundisha na kushauri yanapingana.
Mmoja anakuambia acha kazi mara moja na nenda kwenye biashara,
Mwingine anakuambia anza biashara ukiendelea na kazi.
Mmoja anakuambia usikope fedha kuanza biashara,
Mwingine anakuambia kopa uanze biashara.
Mmoja anakuambia weka kazi usiku na mchana,
Mwingine anakuambia huna haja ya kuweka kazi, tumia tu akili.
Ukiwasikiliza wote unabaki njia panda, unavurugwa, hujui ufanye kipi, hivyo hufanyi chochote.
Ndiyo maana ni muhimu sana ujue unachotaka kwenye maisha yako ni nini, kisha uchague mwalimu au mshauri sahihi kwako na kumsikiliza huyo, huku ukiachana na wengine.

Nenda kapembue maarifa na taarifa utakazokuwa unazifuatilia kuanzia sasa.
Chagua aina ya vitabu utakavyokuwa unasoma.
Na changua mwalimu, kocha na mshauri ambaye utamfuata,
Baada ya kufanya uchaguzi huu, komaa nao mpaka upate kile unachotaka.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania