“You should live your life so that you are not afraid of death, and at the same time do not wish to die.” – Leo Tolstoy
Ishi maisha yako kwa namna ambayo hutahofia kifo, wakati huo huo usitamani kufa.
Watu hufikiri kwamba unapokuwa huhofii kifo basi unakitafuta kije kwako.
Sivyo unavyopaswa kuendesha maisha yako.
Kwanza kabisa hakikisha kila wakati umejiandaa kwa kifo chako, kwa kuiishi kila siku kwa ukamilifu wake, chochote muhimu usikiahirishe.
Lakini pia yalinde sana maisha yako kuepukana na kifo, kwa kuhakikisha unakuwa bora na salama wakati wote.
Ukizingatia hayo mawili, utakuwa na maisha bora sana kila wakati.
Kama ambavyo Seneca amewahi kutuambia, tunapaswa kujiandaa kama tumefika mwisho wa maisha yetu, hatupaswi kuahirisha chochote, tunapaswa kufunga vitabu vya maisha yetu kila siku. Seneca anatuonesha umuhimu wa kuishi kila siku kwa ukamilifu.
Mahatma Gandhi amewahi kusema; Ishi kama vile utakufa kesho, jifunze kama vile utaishi milele. Kauli hii inaleta pamoja namna ya kutokuogopa kifo (kwa kufanya kazi yako vizuri) na jinsi ya kuepuka kufa (kwa kuendelea kujifunza kila siku).
Na Charlie Munger amewahi kusema; Ninachotaka kujua ni wapi nikienda nitakufa, ili niepuke kwenda hapo. Hapa tunajifunza jinsi ya kuepuka kifo, kwa kujua uzembe tunaoweza kufanya ukaleta kifo na kisha tukauepuka.
Rafiki, hofu ya kifo haipaswi kukusumbua kwa namna yoyote ile.
Kwa sababu unakamilisha kila siku yako bila kuahirisha chochote,
Lakini pia una maandalizi mazuri kama utaiona kesho.
Maisha ya mafanikio ni mkusanyiko wa siku ulizoishi kwa mafanikio.
Kaiishi siku hii ya leo kwa mafanikio.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania