Heaven is closer to those people who purify their souls. Those who have only the knowledge received by our five senses do not know the essence of things. The real knowledge is the understanding that there is a higher spiritual force. —INDIAN WISDOM
Kuna nguvu ambayo iko juu yetu,
Nguvu ambayo huwezi kuielezea kwa milango yetu mitano ya fahamu,
Huwezi kuiona, kuisikia, kuigusa, kuinusa wala kuionja.
Lakini nguvu hii ipo na inafanya kazi.
Hii ni nguvu ya kiroho.
Hii ndiyo nguvu inayotuwezesha kujua kiini cha kila kitu.
Ujuzi wa kweli kwenye maisha ni kujua uwepo wa nguvu hii.
Na mbingu ziko karibu kwa wale wanaoijua na kuitumia nguvu hii.
Nguvu hii ina majina tofauti kwa watu tofauti,
Imekuwepo tangu enzi na enzi,
Na imekuwa inatumika pale uwezo wa kawaida wa binadamu unaposhindwa jambo.
Mfano tangu enzi na enzi, kabla dini hazijatufikia, wazee wetu waliamini kwenye mizimu,
Na pale waliposhindwa kutatua matatizo yao, walienda kwenye mizimu na kufanya tambiko na mengine na kwa imani, matatizo waliyokuwa nayo yalitatuliwa.
Kwa sasa tuna dini na mifumo mingine ya imani, ambapo mambo yakitushinda tunarudi kwa Mungu kwa kufanya maombi, na matatizo yetu yanatatuliwa.
Mifano hiyo inatuonesha uwepo wa nguvu ya juu kwenye maisha yetu, nguvu ambayo inaweza kutuvusha kwa chochote tunachopitia.
Hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu kutambua nguvu hiyo na kuitumia vizuri, siyo tu wakati wa magumu, bali kuongozwa na nguvu hii kila wakati na maisha yatakuwa bora sana.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania
Asante kwa kunifundisha nguvu ya kiroho kupitia Imani katika kutenda kazi.
LikeLike