“We understand very clearly that to be a person with high morals is to be a person with a liberated soul. Those who are disappointed or concerned or afraid, or who are involved in passions, cannot free their souls.” —CONFUCIUS

Dhana ya uhuru ni kitu kigumu sana kwa wengi kuelewa.
Wengi hufikiri uhuru ni kufanya kile unachotaka, wakati unapotaka na kwa namna unayotaka wewe.
Na wengi wanapofanya hivyo, wanakuja kugundua hawapo huru, bali wameendelea kuwa watumwa, tena wa miili yao, utumwa ambao ni mbaya sana.

Uhuru sahihi ni zao la maadili,
Unakuwa huru kulingana na maadili uliyonayo.
Unakuwa huru kwa viwango vya udhibiti uliojiwekea mwenyewe.
Hivyo uhuru siyo kupata kila unachotaka, bali kupata kile kilicho sahihi.

Mtu pekee aliye huru kwenye nafsi yake ni yule anayeishi kwa maadili ya hali ya juu.
Kuwa na hali ya kukata tamaa, wasiwasi, hofu na shauku kali ni dalili za kutokuwa huru.
Unapokuwa huru, hakuna chochote kinachokusumbua.
Hata matokeo unayoyapata hayawi usumbufu kwako.
Iwe ni matokeo uliyotaka au ambayo hukutaka.
Uhuru wako uko kwenye kile ulichofanya na siyo kwa matokeo uliyopata.

Chagua leo kuishi kwa maadili ya juu ili uweze kuwa huru kwenye maisha yako.
Chagua leo kipi sahihi kwako kufanya na kipi siyo sahihi.
Kisha jikataze kufanya kile kisichokuwa sahihi hata kama unatamani sana kukifanya.
Usijidanganye na uhuru, bali simamia maadili.
Kwa sababu maadili ndiyo yatakayokuweka huru.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania