“You should celebrate each new day with a good action, a good deed. This is the best way to start a new day.” – Leo Tolstoy

Unapaswa kuishangilia kila siku mpya unayoipata kwa matendo mazuri, kwa kuchukua hatua sahihi.
Njia bora kabisa ya kuianza kila siku yako mpya ni kuchukua hatua sahihi.
Tunaishi kwenye kipindi ambacho kelele na usumbufu ni mwingi mno.
Na wale wanaoendesha kelele na usumbufu huo, wana kila mbinu za kukufikia na kuiba muda wako.
Watakuletea habari mpasuko (breaking news),
Watakuletea udaku wa kila aina kuhush wengine,
Na pia watakupa habari hasi zinazoendelea,
Hapo utaona hupaswi kupita, hivyo kuianza siku yako kwa kufuatilia mambo mbalimbali.
Kwa kuwa usumbufu na kelele ni nyingi, ukishaianza siku yako kwa namna hiyo, huwezi tena kurudi kwenye hali ya kawaida.
Maana mambo mengi zaidi yanaendelea kuja kwako, ambayo unajiaminisha ni muhimu kabisa.

Ili kulinda muda wako na ili kuweza kufanya makubwa kwenye siku yako,
Unapaswa kushika hatamu ya siku yako,
Kuacha kuruhusu wengine kuitumia hovyo,
Na kuhakikisha wewe mwenyewe ndiye unayeitumia siku yako,
Kwa kufanya yale ambayo ni sahihi kwako ili kufika kule unakotaka kufika.
Kila siku mpya unayoipata, ipangilie kabla hujaianza.
Na ukishaianza, unachofuata ni mipangilio yako kwanza na siyo kuhangaika na wanayoleta wengine.

Muda wako na nguvu zako ni rasilimali ulizonazo kwa uhaba mkubwa sana,
Zitumie vizuri kwa kufanya yale yaliyo sahihi kwako badala ya kuacha rasilimali hizo zipotee tu.
Ipokee kila siku kwa kushangilia na kuchukua hatua zilizo sahihi.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania