“Take from a person who follows the divine law everything which other people think of as comfort and wealth, and nevertheless such a person will remain happy.” – Leo Tolstoy

Furaha ya kweli ni ile ambayo haiwezi kuondoka au kuondolewa na chochote.
Hata pale mtu anapopoteza kila alichonacho, bado anaendelea kuwa na furaha.
Furaha hii inatokana na mtu kuzijua kanuni za asili na kuziishi, na kujua kusudi la maisha yake na kulifanyia kazi.
Kwa mtu wa aina hii, kitendo chs yeye kuwa hai, ni furaha kubwa sana kwake.
Kwa sababu uhai wake una mchango mkubwa kwa wengine.
Lakini wale ambao hawazijui kanuni za asili, au hawajui kusudi lao,
Furaha yao inatokana na vitu vya nje.
Mali walizonazo, nafasi na vyeo vyao na hadhi za kijamii walizonazo.
Wanapopoteza vitu hivyo vya nje, wanapoteza utambulisho wao na hapo furaha inapotea.

Hakikisha furaha kwenye maisha yako ni zao pa ndani yako,
Hakikisha furaha uliyonayo inatokana na kulijua na kuliishi kusudi la maisha yako.
Hakikisha furaha hiyo inatokana na kuzijua na kuziishi kanuni za asili.
Na kwa namna hiyo, furaha yako itakuwa na ulinzi mkali,
Hakuna chochote kitakachoweza kuiondoa au kuiondosha.
Na kilicho muhimu pia ni furaha hiyo itakuweka huru, maana haitegemei chochote cha nje yako.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania