“To punish others is like putting more wood in the fire. Every crime already has punishment in itself, and it is more cruel and more just than the punishment created by people.” – Leo Tolstoy
Kwenye maisha kuna watu huwa wanafanya mambo mbalimbali ambayo yanatukwaza au kutuumiza.
Hali hiyo inapotokea, huwa tunakimbilia kuwalipa kwa kile ambacho wamefanya.
Tunatafuta njia ya kuwaadhibu ili na wao waumie kama tulivyoumia sisi.
Japo unaweza kujisikia vizuri kufanya hivyo, haina msaada wowote kwako.
Hivyo epuka sana kulipa ubaya kwa ubaya,
Epuka tamaa ya kulipa kila baya ambalo watu wamekufanyia,
Na achana kabisa na matakwa ya kuwaadhibu wale ambao wamekukosea kwa namna moja au nyingine.
Hii ni kwa sababu;
👉🏼Unapolipa ubaya kwa ubaya unakuwa hujajitofautisha na aliyekufanyia ubaya. Kama mtu amekuumiza, na ukaona hilo siyo sahihi, je wewe kumuumiza ni sahihi? Chochote ambacho mtu akikufanyia amekukwaza, usikilipe, maana utakuwa umekibariki.
👉🏼Unakuwa umempa kile anachotaka. Mtu yeyote anapokukwaza au kukuumiza, raha yake ni kuona umekasirika na wewe ujibu mapigo. Ukifanya hivyo basi lengo lake linakuwa limetimia, lakini ukiachana naye, hilo litamuumiza zaidi kuliko ulivyoumia kwa alichokufanyia.
👉🏼Ni kujishusha hadhi yako. Watu dhaifu huwa wanaona njia pekee ya kuonekana wa muhimu ni kuumiza au kukwaza wengine. Hivyo unapowajibu, unakuwa umejishusha kwenye hadhi yao. Kumbuka usemi kwamba ukipigana na nguruwe, wote mtachafuka, lakini nguruwe atakuwa anafurahia hali hiyo.
👉🏼Wanachokifanya ni adhabu tosha kwao. Hakuna adhabu inayomuumiza mtu kama kosa alilofanya yeye mwenyewe. Hivyo usikimbilie kujibu kila ambacho mtu anafanya kukuumiza, badala yake endelea na maisha yako. Alichofanya kitamuumiza sana mwenyewe.
👉🏼Na mwisho, huna muda huo, wewe mwenyewe unekuwa unasema mambo ni mengi muda mchache, sasa kwa nini uupoteze kuhangaika na watu wanaokukwaza au kukuumiza, achana nao kabisa.
Kwa sababu hizo, achana kabisa na wale wanaokuumiza, kukutesa au kukukwaza kwa namna yoyote ile. Ni adhabu tosha kwako na inakupa wewe muda wa kuhangaika na mambo yako na siyo kuhangaika na watu.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu ASILI NA SOKO, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/07/02/2010
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,