“There’s only one very good life and that’s the life you know you want and you make it yourself.” — Diana Vreeland

Ndani kabisa ya moyo wako, unajua ni maisha ya aina gani unayoyataka.
Unajua kabisa maisha mazuri kwako yakoje,
Unajua nini unapenda kufanya na wapi unataka kufika.
Umekuwa unajua hayo tangu ukiwa mdogo.
Lakini tatizo lilianza pale jamii ilipokuambia unachotaka hakiwezekani,
Ikakuambia usijisumbue na mambo ya kufikirika,
Ikakusisitiza uwe tu kama wengine walivyo.
Na wewe ukaisikiliza jamii,
Na sasa una hasira ndani yako,
Maisha ambayo jamii ilikuambia uyaendeshe huridhiki nayo,
Huku yale uliyokuwa unayataka unaona hayawezekani tena.

Ninachotaka kukuambia leo ni hiki,
Bado hujachelewa kuanza kuyaishi maisha yako,
Usiangalie muda kiasi gani umepoteza,
Bali fanya maamuzi sasa na anza kuyaishi maisha yako.
Achana na kujiandaa kuishi, anza kuyaishi sasa.
Unajua unachotaka,
Unajua cha kufanya,
Anza kufanya,
Na usijali wengine wanafanya au kusema nini.
Wewe pekee ndiye utakayeyaishi maisha yako,
Kuna maana gani kuishi maisha ambayo huridhiki nayo?

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kushinda mabishano, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/07/04/2012

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,