“Work is of two kinds: first, altering the position of matter at or near the earth’s surface relatively to other such matter; second, telling other people to do so. The first kind is unpleasant and ill paid; the second is pleasant and highly paid.” – Bertrand Russell
Kazi imegawanyika kwenye aina kuu mbili,
Aina ya kwanza ni kufanya kazi husika, yaani kuweka nguvu na juhudi kwenye kutekeleza jukumu husika.
Na aina ya pili ni kuwaelekeza watu wengine kufanya kazi husika, hapa unaweka nguvu na juhudi zako kuwaelekeza na kuwasimamia wengine kutekeleza jukumu husika.
Aina hizi mbili za kazi huwa hazilingani,
Aina ya kwanza inachosha na malipo yake ni kidogo,
Aina ya pili haichoshi na malipo yake ni makubwa.
Aina ya kwanza haina nyenzo, huku aina ya pili ikiwa na nyenzo kubwa.
Mfano kwenye kilimo, wewe kuingia shambani na kulima mwenyewe ni aina ya kwanza ya kazi. Kuweka watu wengine walime ni aina ya pili ya kazi.
Kwenye biashara, wewe kukaa kwenye biashara na kuuza mwenyewe ni aina ya kwanza ya kazi, kutengeneza timu nzuri ya mauzo ni aina ya pili.
Kadhalika kwenye kampuni, mkurugenzi mkuu analipwa zaidi kuliko wafanyakazi wanaofanya majukumu husika.
Aina ya kwanza ya kazi haina nyenzo kwa sababu inategemea nguvu zako, muda wako na ujuzi wako, vitu ambavyo vina ukomo. Una masaa 24 tu kwa siku, na huwezi kufanya kazi muda wote. Kadhalika huwezi kujua kila kitu.
Aina ya pili ya kazi ina nyenzo za kila aina, unaweza kutumia muda wa wengine, nguvu za wengine na ujuzi wa wengine kufanya makubwa zaidi.
Badala ya kufanya kazi mwenyewe kwa msaa 10 kwa siku, unaweka watu 10 ambao kila mmoja anafanya kazi masaa 10 kwa siku, unapata masaa 100 ya kazi kwa siku badala 10.
Unapata ujuzi wa aina mbalimbali kulingana na hitaji la kazi, ambapo siyo lazima wewe uwe na ujuzi huo.
Kwa kila unachofanya, pambana kufikia aina ya pili ya kazi.
Wengi tunaanzia kwenye aina ya kwanza ya kazi,
Lakini hatupaswi kudumu hapo,
Pambana kufika kwenye aina ya pili,
Kwa sababu kadiri muda unavyokwenda ndivyo unavyozidi kuchoka,
Ukitaka ufanye aina ya kwanza ya kazi maisha yako yote, huwezi kufikia mafanikio makubwa.
Hakuna aliyefikia mafanikio makubwa kwa kufanya aina ya kwanza ya kazi pekee.
Wote wenye mafanikio makubwa wanafanya aina ya pili ya kazi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu wakati sahihi wa kuanza, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/07/12/2020
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
Asante kocha, kwa hakika hii aina ya kwanza ya kazi pekee haiwezi kukufikisha kwenye mafanikio makubwa hapa naona umuhimu wa kupambana ili kutoka kwenye aina ya kwanza ya ajira na kuwa kwenye aina ya pili ya ajira.
asante.
LikeLike
Vizuri Joseph, kila la kheri katika mapambano hayo.
LikeLike
Asante kocha,kwa tafakari zinazofungua ufahamu kila siku.
LikeLike