“You will never be happy if you continue to search for what happiness consists of. You will never live if you are looking for the meaning of life.” – Albert Camus
Njia ya uhakika ya kukosa furaha kwenye maishs yako, ni kutumia muda wako kuitafuta furaha kwenye maisha.
Furaha ni kana kipepeo, ukiimbiza inazidi kwenda mbali, ukiachana nayo inakufuata yenyewe.
Unapojiwekea lengo kwamba unafanya kitu fulani ili upate furaha, jua hakuna namna unaweza kufikia furaha hiyo.
Njia ya uhakika ya kushindwa kuyaishi maisha yako ni kutumia muda wako kutafuta maana ya maisha.
Kila wakati utakapofanya zoezi hilo utakuja na majibu tofauti,
Na hivyo utakosa msimamo kwenye maisha yako.
Jawabu la uhakika la maisha yako ni moja, KUYAISHI.
Jukumu lako ni kuyaishi maisha yako,
Achana na mahangaiko ya furaha au maana,
Wewe kabiliana na kile kilicho mbele yako,
Sikiliza nafsi yako, inajua mengi kuhusu wewe,
Chochote unachofanya, weka kila ulichonacho kwenye kitu hicho.
Utakachogundua ni kwamba!
Furaha ni matokeo ya wewe kuyaishi maisha yako,
Maana ya maisha yako ni namna unavyoyaishi.
Kwa kuacha kuhangaika na vitu hivyo viwili na kukazana kuyaishi maisha yako, vinakuja kwako vyenyewe.
Hivyo kama unalalamika maisha yako hayana furaha,
Kama unaona maisha yako hayana maana,
Ni kwa sababu unatumia nguvu sana kwenye kutafuta vitu hivyo.
Hebu achana navyo na weka mkazo kwenye kuyaishi maisha yako kwa ukamilifu.
Na vitu hivyo vitakuja kwako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu matatizo ya kutengeneza, fungua hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/07/18/2026
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,