“It’s impossible to begin to learn that which you think you already know.” – Epictetus
Hatua ya kwanza ya kujifunza ni kujua kwamba hujui.
Ukiwa mjuaji, huwezi kujifunza.
Na ujuaji umekuwa kikwazo kwa wengi,
Wanafikiri wanajua kila kitu hivyo hawana tena cha kujifunza.
Wakati mwingine wanajua hawajui, lakini hawataki kuonekana hawajui, hivyo wanajifanya wanajua.
Usiwe na tabia hizo,
Kila wakati kuwa tayari kujifunza,
Hata kama kitu unakijua, jifunze tena, utakijua kwa undani zaidi.
Kila unayekutana naye jua kuna anachojua ila wewe hujui,
Kuwa mnyenyekevu na jifunze.
Na unapojifunza, ndipo unazidi kuona ni vitu vingi kiasi gani hujui.
Hilo litakufanya uwe mtu wa kujifunza kila siku.
Kwa sababu kujifunza hakuna mwisho,
Na kwa zama tunazoishi sasa, huna sababu ya kueleza kwa nini hujifunzi,
Maana maarifa yanapatikana kwa urahisi kuliko kipindi chochote kile.
Hivyo kila siku tenga muda wa kujifunza kitu kipya.
Kujifunza ndiyo uwekezaji ambao ukiufanya utakulipa sana,
Kwa sababu ukishajua kitu, hakuna anayeweza kukunyang’anya ujuzi huo.
Weka kipaumbele kwenye uwekezaji huu muhimu.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kushindwa kabla hujaanza, soma; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/07/19/2027
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,