“Watch her carefully right now,” she said, “because she’s teaching you how to live.” – Anne Lamott, Bird by Bird
Kwenye kitabu chake kinachoitwa Bird by Bird mwandishi Anne Lamott anatushirikisha kisa cha rafiki yake aliyefariki kwa saratani.
Miezi sita kabla ya kifo cha rafiki yake, Anne alikuwa anawasiliana na daktari wake kujua kama kuna habari zozote nzuri na kitu anachoweza kufanya kumsaidia rafiki yake.
Daktari huyo hakuwa wa kupindisha maneno, alimweleza wazi kwamba kwa hali aliyonayo rafiki yake hawezi kupona.
Lakini kuhusu afanye nini, alikuwa na ushauri mzuri sana kwake.
Alimwambia mwangalie rafiki yako jinsi anavyokufa, atakufundisha jinsi ya kuishi.
Nafikiri huu ni moja ya ushauri bora kabisa unaoweza kumsaidia mtu kwenye maisha yake.
Ukitaka kujua thamani halisi ya kitu, jifunze kwa wale ambao wanakipoteza kitu hicho.
Pia tunapowapoteza watu wetu wa karibu, badala ya kuumia na kujilaumu labda kuna kitu tungeweza kufanya, tunapaswa kujifunza kwao jinsi ya kuishi maisha yetu.
Kupitia mateso wanayopitia watu wetu wa karibu, tunapaswa pis kujifunza jinsi ya kuishi maisha yetu ili tusipitie wanachopitia wao.
Kama una mtu wa karibu ambaye ameathiriwa sana na ulevi kitu kilichopelekea kuharibu maisha yake, achana kabisa na ulevi.
Kama una mtu wa karibu ambaye ametumbukia kwenye madeni na yamekuwa kaburi lake, epuka madeni kama ukoma.
Dunia ni darasa tosha kwetu,
Kwa kila anayetuzunguka tuna mengi ya kujifunza,
Tuchukue hatua ya kujifunza na kufanyia kazi yale tunayojifunza na maisha yetu yatakuwa bora kabisa.
Huwa nasema kama huna mtu wa karibu aliyefanikiwa wa kujifunza kwake, chagua mtu wa karibu aliyeshindwa na jifunze kwake, angalia kila alichofanya kwenye maisha yake, kisha wewe fanya kinyume na alivyofanya yeye.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu unataka kuwa nani, soma; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/07/21/2029
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
Wakati nasoma ukurasa huu nimeyatafakari mengi hasa niliyoyapitia,ninayoyapitia na maisha ya watu wa karibu wanaonizunguka,hasa nimepata darasa na somo la kutosha , nitaendelea kuyafanyia kazi kwa umakini sana.
LikeLike
Vizuri Beatus.
LikeLike