“In a memorable example, Dawes showed that marital stability is well predicted by a formula: frequency of lovemaking minus frequency of quarrels You don’t want your result to be a negative number.”
― Daniel Kahneman, Thinking, Fast and Slow

Kwenye kitabu chake kinachoitwa Thinking, Fast and Slow mwandishi Daniel Kahneman anatushirikisha kwamba, katika kufanya maamuzi, kutumia kanuni ni bora kuliko kutumia hisia na mazoea.
Hiyo ni kwa sababu unapotumia hisia na mazoea unachukua taarifa za juu juu na unaweza usione uhalisia. Matokeo huwa yanabadilika kulingana na hisia zako wakati unafanya maamuzi.
Lakini unapotumia kanuni, haiathiriwi na chochote, kila wakati inaleta matokeo sahihi.

Akashirikisha kanuni ya kuweza kutabiri kudumu kwa ndoa,
Kanuni hiyo inasema kudumu kwa ndoa = IDADI YA KUFANYA MAPENZI – IDADI YA KUGOMBANA.
Namba ikiwa hasi, hiyo ndoa au mahusiano yako hatarini.
Mfano kama kwa wiki wanandoa wanafanya mapenzi mara mbili, huku wakigombana mara tatu, kwa kanuni 2 – 3 = -1
Jibu ni hasi moja, kiashiria kwamba ndoa ipo hatarini.

Hii inaeleza vizuri kwa nini ndoa na mahusiano huvunjika kwa urahisi pale watu wanapokuwa mbali na wenza wao.
Kwa kuwa migogoro midogo midogo huwa haikosekani, na huku umbali ukiondoa au kupunguza ufanyaji wa mapenzi, namba inakiwa hasi.
Namba hiyo inapokuwa hasi kwa muda mrefu, ndoa au mahusiano yanavunjika.

Tumia kanuni hii kujipima kila mara na hakikisha jibu unalopata halowi hasi, yaani idadi ya kugombana haipaswi kuzidi idadi ya kufanya mapenzi.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu unachokasirikia kinachekesha, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/07/22/2030

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,