“I guard my treasures: my thought, my will, my freedom. And the greatest of these is freedom.” – Ayn Rand

Fikra, utashi na uhuru, ni hazina ambazo kila mmoja wetu anazo.
Hazina ambazo mtu ukiweza kuzitumia vizuri, zinakupa kila unachotaka.

Na katika hazina hizo, uhuru ndiyo hazina iliyo juu kabisa.
Ni hazina ya kipekee,
Hazina ambayo kila mtu anazaliwa nayo.
Lakini cha kushangaza, ni wachache sana wanaojua wana hazina hii na kuweza kuitumia.

Jamii haitaki ufikiri kwa akili yako, bali inataka ufikiri kama wengine na uamini kile wanachoamini.
Jamii haitaki utumie utashi wako, bali inataka ufuate mkumbo, kama una kitu cha tofauti inakufanya ujione unakosea.
Jamii haitaki uwe huru, bali inataka ikutawale ili uwe kama wengine.

Njia pekee ya kuishi maisha yako kwa ukamilifu ni kutambua na kutumia hazina hizo tatu,
Tumia fikra zako,
Tumia utashi wako,
Kuwa huru.

Vitu hivyo hutapewa na yeyote, tayari vipo ndani yako, ni wewe uanze kuvitumia.
Huna cha kusubiri, anza kuvitumia sasa.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa leo ni kuhusu mambo mbalimbali ya kuzingatia kwenye maisha, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/07/31/2039

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani.