“For the most part, false and harmful opinions are distrib uted and supported by influence. We are too likely to accept the views and thoughts of other people without trying to investigate them deeper and further ourselves. Unimportant people are those who accept other people’s thoughts without developing them themselves.” – Leo Tolstoy
Uongo huwa unavumishwa na kuwa maarufu, watu wengi wanakubaliana nao na baada ya hapo unachukuliwa kama ukweli.
Kwa sababu wengi wanakubaliana na uongo huo, nguvu ya kundi inawafanya wale wasioamini uongo huo kuonekana wana matatizo.
Kadiri kundi linavyozidi kuwa kubwa, ndivyo uongo unavyozidi kukuzwa.
Kama unataka kuujua na kuusimamia ukweli, basi usifuate kundi.
Kwa jambo lolote, usiamue kufuata wengi wanasema au kufanya nini,
Badala yake fikiria kwa akili yako mwenyewe,
Jifunze, angalia wengine wanafanya nini na angalia kila kinachoendelea.
Kisha fikiri kwa akili yako mwenyewe na fikia maamuzi yako mwenyewe.
Tambua wengi waliopo kwenye kundi wamejikuta kwenye kundi hilo bila ya kufikiri wao wenyewe.
Kwa sababu kundi ni kubwa na maarufu, watu wanaanini litakuwa sahihi na hakuna haja ya kuhoji au kudadisi.
Huwezi kuwa huru kama utakuwa mtu wa kufuata makundi.
Utakuwa huru kwa kufikiri mwenyewe na kutumia akili yako katika maamuzi.
Nguvu ya kujifunza, kufikiri na kufanya maanuzi iko ndani yako, usiiache ikadumaa, badala yake itumie vizuri.
Tahadhari; unapofikiri na kufanya maamuzi ambayo ni ya tofauti na kundi kubwa, huna haja ya kubishana nao, wala kuwaonesha wamekosea na wewe uko sahihi.
Kumbuka lile ni kundi kubwa, hata uwe na hoja kiasi gani, huwezi kulishinda kwa ukubwa wake na muda utakaotumia kubishana nao, ni muda unaopoteza, ambao ungeweza kuutumia vizuri zaidi.
Hivyo fikiri kwa akili yako, fanya maamuzi sahihi na fanya mambo yako kwa namna bora.
Waache wengine waendelee na yao, wapo watakaoona unapata matokeo ya tofauti, watakuja kwako kutaka kujifunza, kama ukiwapima na kuona wako tayari kupokea ukweli, basi wape ukweli.
Kama utawapa ukweli na kuupinga, usitumie hata sekunde moja kubishana nao au kujitetea, badala yake kubaliana nao na wasihi waendelee na kundi kama linawapa matokeo bora zaidi.
Na wewe endelea na yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kuomba samahani na kutokutoa visingizio, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/08/04/2043
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani.