The goodness which you do gives you pleasure, but not satisfaction. No matter how much goodness you do, you should wish to do more and more. —Confucius
Unapotenda wema, tenda kwa sababu ndiyo asili yako na siyo kwa sababu kuna kitu unachotaka kufanya.
Ukitenda wema kwa mategemeo ya kupata kitu fulani itapelekea wewe kufikia ukomo kwenye wema wako.
Kwa kuwa wema hautakupa kile unachotegemea kupata, utaona hakuna haya ya kuwa mwema.
Utaweka ukomo kwenye wema wako.
Utaanza kutokuwa mwema na atakayeathirika na kuumia zaidi ni wewe mtendaji, siyo unayemtendea.
Unapaswa kutenda wema kwa sababu ndiyo msingi wa maisha yako, ndiyo namna umechagua kuishi.
Manufaa pekee ya wewe kutenda wema ni pale unapoutenda, ukijua umefanya jambo jema, umeishi kwa misingi yako
Usitende wema ukitegemea kitu kingine zaidi ya hicho.
Usitegemee kusifiwa na wengine kwa wema uliotenda.
Usitegemee hata yule uliyemtendea wema akupe shukrani.
Usitegemee kutumia wema huo kudai kitu fulani baadaye.
Ukitenda wema kwa sababu hizo, tayari umepotoka,
Hautakuwa tena wema, kwa sababu utakwazika pale utakapokosa vile ulivyotegemea.
Nenda katende wema leo na kila siku, kwa sababu ndiyo maisha uliyochagua kuishi.
Wengine wanasema na kufanya nini haikuhusu, kilicho muhimu kwako ni kutenda wema.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu vitu viwili usivyopaswa kukosa, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/08/16/2055
Pia kama hujafanya tathmini ya juma lako, fungua kufanya, pia soma tathmini za wengine, kuna mazuri mengi ya kujifunza na ushauri mzuri unaoweza kufanyia kazi pia, fungua hapa; http://www.mafanikio.substack.com/p/tathmini-ya-juma-la-332020/comments
Kwa maarifa mbalimbali niliyokutana nayo juma lililopita, fungua hapa; http://www.mafanikio.substack.com/p/mazaga-ya-juma-la-342020/comments
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.