“Winning is great, sure, but if you are really going to do something in life, the secret is learning how to lose. Nobody goes undefeated all the time. If you can pick up after a crushing defeat, and go on to win again, you are going to be a champion someday.” – Wilma Rudolph

Siri kuu ya mafanikio makubwa kwenye maisha yako, ni kujifunza jinsi ya kushindwa.
Na siyo kujifunza namna ya kushindwa unachofanya,
Bali kujifunza namna ya kuinuka tena baada ya kuanguka na kushindwa.

Kila mtu huwa anapitia hali ya kushindwa kwenye maisha yake.
Kinachowatofautisha wanaofanikiwa na wanaoshindwa ni jinsi wanavyopokea kushindwa kwao.

Wanaofanikiwa wanapokea kushindwa kama sehemu ya kujifunza na kuwa bora zaidi.
Wanaangalia nini kimepelekea washindwe na kisha kufanya kwa ubora zaidi wakati mwingine.

Ambao hawafanikiwi huwa wanachukulia kushindwa kama adhabu ya mwisho,
Wanaona ndiyo ukomo wao, hakuna wanachoweza kukifanya tena hapo.
Wanapojaribu kitu wakashindwa, wanachukulia ndiyo hatima ya maisha yao, hawajaribu tena kitu hicho kwa ubora zaidi.

Chagua kuwa upande wa ushindi,
Kwa kujifunza jinsi ya kushindwa,
Na kutumia kushindwa kwako kama ngazi ya kufanikiwa zaidi.
Hakuna asiyeshindwa kwenye maisha.
Kinachotutofautisha ni jinsi tunavyopokea na kukabiliana na kushindwa.

Na kushindwa ni ishara kwamba unajaribu mambo mapya na makubwa.
Wajibu wako ni kujifunza na kufanya kwa ubora zaidi.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu mbinu nne za kufikia mafanikio makubwa kwa muda mfupi, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/09/04/2074

Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.