“What is not clear should be cleared up. What is not easy to do should be done with great persistence.” —Confucius

Kama kuna kitu ambacho hukielewi, usikiache na kwenda kwenye vile unavyoelewa,
Badala yake ng’ang’ana mpaka ukielewe.
Mambo mazuri na muhimi huwa hayaeleweki haraka,
Ndiyo maana wachache mno ndiyo wanaoyaelewa na kunufaika nayo.

Kama kuna kitu ambacho siyo rahisi kufanya usiache kukifanya na kukimbilia vitu rahisi.
Badala yake ng’ang’ana kukifanya kwa msimamo mpaka pale kinapogeuka tabia na kuwa rahisi kufanya.
Mambo mazuri na yenye manufaa huwa siyo rahisi kufanya, na ugumu wa mambo hayo ndiyo unaowazuia wengi wasifanikiwe.
Lakini uzuri ni kwamba kama utang’ang’ana kufanya, baadaye yanageuka kuwa rahisi na inakuwa tabia kabisa.
Na hapo unajitofautisha na wale wasiohimili magumu.

Kila unapokutana na ugumu, hisia za kwanza kukujia ni kuacha na kukimbia, lakini usizisikilize,
Wewe jua magumu hayo yana manufaa makubwa ndani yake, hivyo ng’ang’ana kufanya na utanufaika sana.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu adui mmoja ni maadui wengi, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/10/03/2103

Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.