“The cause of anger is the sense of having been wronged, but one ought not trust this sense. Don’t make your move right away, even against what seems overt and plain; sometimes false things give the appearance of truth.” – Seneca
Hasira huwa ni zao la hisia, pale unapoamini kwamba umefanyiwa isivyo sahihi.
Lakini siyo mara zote hisia zako zinakuwa sawa.
Kuna wakati hisia huwa zinachochewa kimakosa, kutokana na mtazamo usiokuwa sahihi unaokuwa nao.
Ili kuepuka kufanya mambo kuwa magumu zaidi, epuka kukimbilia kuchukua hatua yoyote unapokuwa na hasira.
Ukishajiona una hasira, jipe muda kwanza, usikimbilie kujibu au kufanya lolote.
Acha hasira zako zitulie na hapo utaliona jambo kwa namna ya tofauti kabisa.
Kinachotusumbua siyo yale yanayotokea, bali namna tunavyoyatafsiri yanayotokea.
Pale jambo lolote linapotokea, huanza kwa kuibua hisia ndani yako kabla hata hujafikiri.
Ukijifunza kujidhibiti katika hali hizo, utajiepusha na matatizo mengi.
Asubuhi ya leo tafakari hatua ambazo umewahi kukimbilia kuchukua ukiwa na hasira na ona madhara yake ya baadaye yalivyokuwa makubwa zaidi.
Kuanzia sasa jiambie hutakuwa mtu wa kukimbilia kuchukua hatua pale unapokuwa na hasira, jipe muda na mambo yatakwenda vizuri.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kuiangalia asili pale unapojikuta njia panda, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/10/15/2115
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.