“Whatever fate befalls you, do not give way to great rejoicings or great lamentation; partly because all things are full of change, and your fortune may turn at any moment; partly because men are so apt to be deceived in their judgment as to what is good or bad for them.”
— Arthur Schopenhauer
Kitu kimoja kuhusu binadamu ni jinsi ambavyo huwa tunajisahau haraka,
Hicho ndiyo kimekuwa chanzo cha matatizo mengi tunayopitia.
Pale mambo yanapokuwa mazuri kwa mtu, anajisahau na kuona yataendelea hivyo hivyo.
Mambo yanabadilika ghafla na yanamkuta hajajiandaa, hivyo anajikuta kwenye ugumu mkubwa.
Pale mambo yanapokuwa mabaya mtu anakata tamaa na kuona hivyo ndivyo maisha yake yatakavyokwenda,
Kwa kukata tamaa anashindwa kuzitumia vizuri fursa zinazojitokeza.
Haijalishi uko kwenye hali gani sasa, jua mambo yatabadilika
Hivyo badala ya kujisahau pale ulipo sasa, kuwa na maandalizi sahihi kwa mabadiliko yoyote yanayoweza kuja kwako.
Usishangilie sana pale mambo yanapokuwa mazuri na wala usilalamike sana pale mambo yanapokuwa mabaya.
Zote hizo ni hali za muda tu, zitumie wakati unazipitia huku ukijua kuna mabadiliko yanakuja, hali hizo hazidumu milele.
Na hata pale jambo lolote linapotokea, usikimbilie kusema ni jambo zuri au baya.
Kugawa mambo kwa uzuri na ubaya kutakupoteza pia.
Badala yake kwenye kila jambo angalia ni kwa jinsi gani unaweza kulitumia.
Usiangalie uzuri au ubaya, bali angalia matumizi.
Kwa kila jambo, kuna namna unaweza kulitumia kwa ubora zaidi.
Muhimu ni usijisahau, maana mambo yanabadilika kila wakati.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kunasa kama sumaku, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/12/04/2165
Rafiki yako anayekupenda sana.
Kocha Dr Makirita Amani.