“Our advice is that every man should remain in the path he has struck out for himself, and refuse to be overawed by authority, hampered by prevalent opinion, or carried away by fashion.” – Johann Wolfgang von Goethe
Ili uweze kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako, lazima ujue kile hasa unachotaka na jinsi gani ya kukipata.
Ukishajua hilo, kaa kwenye njia ya kukufikisha unakotaka kufika na jipe muda.
Njia yoyote utakayochagua kutumia, kuna watu watakushawishi siyo njia sahihi.
Wapo watakaotumia mamlaka waliyonayo kukuzuia au kukukataza.
Wapo watakaokuja kwako na maoni mbalimbali kwa nini njia yako siyo sahihi,
Na pia ni rahisi kwako kushawishika kwa kuangalia wengine wanafanya nini, ukaona kinachofanywa na wengi ndiyo kilicho sahihi.
Usikubali kubabaishwa kwa namna hii.
Njia uliyochagua wewe ndiyo sahihi kwako na itakufikisha kwenye mafanikio makubwa.
Kikubwa ni uwe na subira na kujipa muda, usihangaike na mambo mengi, weka juhudi kwenye njia uliyoichagua.
Ni rahisi kuona njia nyingine ni rahisi kuliko yako, lakini ni mpaka uingie ndiyo utaona ugumu wake.
Pambana na njia uliyochagua na waache wengine wapambane na njia zao.
Usiwe mtu wa kuyumbishwa yumbishwa n wengine.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kufanya kitu kwa kupenda na siyo kuangalia matokeo, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/12/21/2182
Rafiki yako anayekupenda sana,
Kocha Dr Makirita Amani.