Kujifunza kitu mara moja haitoshi, unahitaji kurudia rudia. Kufanya kitu mara moja haikufikishi kwenye mafanikio makubwa, unapaswa kufanya mara kwa mara, kwa muda mrefu.

Hapo ndipo inapokuja changamoto ya mazoea. Kwa sababu umekuwa unajifunza kitu kwa kurudia, unajiambia tayari unajua. Kwa sababu umekuwa unafanya kila siku, unajikuta ukifanya kwa mazoea.

Mazoea ni kikwazo kikubwa kwenye mafanikio, huwezi kufanikiwa kama huheshimu unachofanya. Unapoanza kitu kwa mara ya kwanza unakiheshimu na kuweka umakini wako wote na unakifanya vizuri. Unapoweka mazoea unafanya vibaya.

Usikubali kabisa kuingia kwenye mazoea, kila unachojifunza na kufanya, kiheshimu kweli. Ona kama ndiyo mara ya kwanza na mwisho, weka umakini wako wote hapo.

Kwa wale unaojifunza kwao, waheshimu, hilo litakusaidia kuelewa zaidi.

Ukurasa wa leo ni kuhusu jehanamu unayoishi nayo, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/01/16/2208

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma