Ziada ni mbaya, chochote unachofanya au kuwa nacho kwa ziada huwa kinakulevya na kukupa kiburi. Unaona tayari umeshapata kila kitu.

Uhaba nao ni mbaya, kwa sababu unachokosa unakihofia na kukuweka kwenye hali ya kutawaliwa na wale wanaoweza kukupatia unachokosa.

Mpango mzima ni kuwa na kiasi, kufikia kiasi. Kwa kiasi, huna uhaba na hivyo hofu au kutawaliwa havikusumbui na pia huna ziada hivyo ulevi na kiburi havikukwamishi.

Kwa kila tunayofanya, tuwe na kiasi.

Ukurasa wa kusoma ni kuhusu kinapopatikana unachotafuta, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/01/25/2217

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma