Ukweli unahitaji ushahidi halisi, unaoonekana na kuweza kupimika na kila mtu.

Ukweli unapaswa kuwa kweli kwa kila mtu na kila mahali. Ukweli ambao mtu analazimishwa kuamini bila ya ushahidi siyo ukweli huo.

Kabla ya kukua kwa sayansi, watu waliamini mambo mengi ambayo siyo kweli. Dini na ushirikina viliwaweka watu kwenye hofu kubwa kupitia yale walilazimisha watu waamini.

Lakini sayansi imeleta mwanga, na vingi vimethibitishwa kwamba siyo kweli. Watu waliuawa kwa sababu tu ya kile watu waliamini, ambacho hakikuwa kweli.

Sasa tuna kila nyenzo ya kutuwezesha kuhoji, kudadisi na kupima kila tunachoambiwa au kukutana nacho kama ni kweli.

Tusikubali kulazimishwa kuamini chochote ni kweli bila ya ushahidi. Tusikimbilie tu kukubali na kuamini, bali tuangalie ushahidi uliopo unaoonesha ni kweli.

Ukurasa wa kusoma ni kuhusu kuwa makini na motisha unaotoa, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/01/29/2221

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma