Watu huwa wanajaribu kukuweka kwenye mashindano ya kila aina.

Na ndani yetu binadamu, huwa tuna roho ya kupenda kushindana.

Ila tatizo kubwa la mashindano hayo ni hata ukishinda, hakuna unachonufaika nacho.

Unaweza kubishana na watu na ukawashinda, lakini hutakuwa umewabadili.

Unaweza kushindana kibiashara na kuona umeshinda, lakini kiuhalisia hujashinda.

Tatizo la mbio za panya ni hata ukishinda, unabaki kuwa panya.

Hivyo ushindi wa uhakika ni kutoka kabisa kwenye mbio hizo.

Jiepushe mno na mashindano unayoshawishika kuingia, yanakuondoa kwenye njia sahihi kwako kufika unakotaka.

Kama hutaki kuwa panya, usishiriki kwenye mbio za panya.

Ukurasa wa kusoma ni kuhusu maisha yanayogusa maisha mengine, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/02/03/2226

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma