Kabla hujaruhusu jambo lolote likusumbue au kukupa wasiwasi, jua kwanza kama lipo ndani au nje ya uwezo wako.

Lililo ndani ya uwezo wako ni lile unaloweza kuchukua hatua na ukalibadili na lililo nje ya uwezo wako ni lile ambalo hakuna hatua unaweza kuchukua.

Mfano umetoka nyumbani kuna mahali unataka kuwahi, unafika njiani na kukutana na foleni ndefu ambayo haisogei kabisa, magari yamesimamishwa kupisha msafara wa viongozi fulani, haijalishi una haraka kiasi gani, kuhangaika na hilo hakutabadili chochote.

Kulalamikia hali hiyo hakutaibadili. Badala yake unapaswa kutambua iko nje ya uwezo wako, kuikubali na kutumia muda huo kufanya vitu vingine, mfano kusoma kitabu wakati unasubiri foleni hiyo iishe.

Mstoa Epictetus alisema jukumu letu kwenye maisha ni kujua yaliyo ndani ya uwezo wetu na kuuashughulikia na yaliyo nje ya uwezo wetu na kuachana nayo. Chukua hatua hii kwa kila linalokusumbua.

Ukurasa wa kusoma; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/02/20/2243