Kama unayataka mafanikio makubwa, lazima ujijengee msimamo kwenye kile unachofanya.

Hakuna utakachofanya mara moja ukafanikiwa, ila kile unachofanya kwa kurudia rudia ndiyo utafanikiwa.

Kuandika makala moja siyo jambo la kishujaa, ila kuandika kila siku kwa muda mrefu kutakufanya mwandishi bora.

Kila mtu anaweza kufanya kitu mara moja, ila wanaofanikiwa wanajijengea tabia ya kufanya kila siku kitu kinachowapa msimamo mkubwa wa mafanikio.

Kwa kuwa huna muda wa kufanya mengi, chagua machache muhimu utakayojijengea msimamo kwenye ufanyaji wake.

Ukurasa wa kusoma ni mashindano yasiyo na zawadi, soma; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/03/04/2255

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma