Sehemu ambayo wengi wanayapoteza maisha yao ni kwenye kujiandaa kuishi. Kila wakati mtu anajiambia hajawa tayari, hivyo hafanyi kile anachotaka.

Ukiwa shule unasema ukihitimu utaanza kuishi maisha yako. Ukihitimu unasema ukipata kazi utaanza.

Ukipata kazi unasema ukimaliza kulea utaanza. Ukimaliza kulea unasema ukistaafu utaanza. Ukistaafu unakuta muda umeshakuacha.

Seneca amewahi kusema wapumbavu wanafanana kwenye jambo moja, kila wakati wanajiandaa kuishi na wanaondoka hawajayaishi maisha yao.

Usiwe mpumbavu, maandalizi yametosha sasa, chagua kuyaishi maisha yako kila wakati.

Ukurasa wa kusoma ni jinsi unavyojisumbua mwenyewe, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/03/07/2258

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma