Mafanikio huwa hayaji kwa kuanza kufanya vitu na kuishia njiani, bali huja kwa kufanya vitu mpaka mwisho.

Japo haitakuwa rahisi, japo utakutana na vikwazo na changamoto, huwezi kufanikiwa kama utaishia njiani.

Chochote unachochagua kufanya, amua kukifanya mpaka mwisho wake, kamwe usikubali kuishia njiani, pambana kwa kila namna uendelee kufanya.

Moja ya njia za kufanikiwa ni kuwa na msimamo kwenye kile unachofanya, msimamo huo unaifanya dunia iwe tayari kukupa kile unachotaka.

Wapangaji ni wengi, waanzaji ni wengi pia, ila wakamilishaji ni wachache na ndiyo wanaopiga hatua.

Kuwa mkamilishaji, jitoe kuendelea kufanya bila kujali nini kinaendelea na utafanya makubwa.

Ukurasa wa kusoma ni kuhusu kutumia thamani badala ya uhaba, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/03/10/2261

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma