
Kutokujua hasa kile unachotaka, kutokujitoa hasa kupata unachotaka na kuwa na mbadala ni vikwazo vikubwa vitatu kwa mafanikio yako.
Kama hujui kile unachotaka, kila mara utayumbishwa na wanayofanya wengine, ukiona wanafanya hiki na wewe unajaribu, wakifanya kile unajaribu pia.
Mwisho wa siku unakuta muda umeenda na hakuna cha tofauti umepata.
Kama hujajitoa hasa kufanya ulichochagua, usumbufu wa kila aina utakuingilia, utashawishika na wale wanaotaka kuteka umakini wako, kwa sababu haujatekwa na kile ulichochagua wewe.
Na kama una mbadala na machaguo mengi, kila mara utakuwa unaahirisha yale muhimu na kufanya mbadala wake, kuondokana na hili, usijipe anasa ya machaguo mengi au mbadala, panga kufanya kitu kimoja tu kwa wakati na fanya hicho au usifanye chochote.
Kwa kuzingatia haya matatu, utaokoa muda na nguvu zako nyingi zisipotee kwa yasiyo muhimu.
Ukurasa wa kusoma ni kuangalia wengine kunavyokuwa kikwazo kwako, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/03/11/2263
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma