
Fikra zako zina nguvu ya kuumba chochote kile, kiwe kizuri au kibaya.
Ni wajibu wako kutumia nguvu hiyo ya fikra kutengeneza ndoto kubwa na nzuri kwako na kuziamini kisha kuzifanyia kazi.
Hata kama umefungwa kimwili au mwili unateswa, usiruhusu akili na fikra zako zifungwe au kuteswa.
Hata kama unapitia magumu kiasi gani, usikubali fikra zako ziwe zinaona magumu hayo pekee.
Zifanye fikra zako kuwa rasilimali muhimu kwako na siyo kikwazo kwako.
Fikiri kwa uhuru, ukubwa na usahihi.
Ukurasa wa kusoma ni mapema ni sasa, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/03/19/2270
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma