2276; Kamata tamaa zao…

Huwa hatuzipendi hisia hasa wakati wa maamuzi, lakini hatuwezi kufanya maamuzi yoyote bila hisia.
Hili limethibitishwa kisayansi, baadhi ya watu waliofanyiwa upasuaji wa ubongo na eneo la hisia kuharibiwa, waliweza kufikiri vyema kabisa, lakini hawakuweza kufanya maamuzi.
Chukua mfano mtu anaenda kwenye mgahawa na kuangalia vyakula vilivyopo, ambao eneo la hisia limeharibiwa, mtu anajikuta akipitia kila kilichopo lakini anashindwa kuchagua kipi atakula.
Lazima kuwe na hisia fulani zinazokusukuma mtu ili uweze kufanya maamuzi.
Na katika kuwashawishi wengine, lazima ujue hisia zao ambazo ukizigusa watasukumwa kukubaliana na wewe.
Baadhi ya hisia ambazo zimekuwa zinawasukuma wengi kwenye maamuzi ni hizi;
1. Kutambuliwa na kuheshimiwa na wengine.
2. Kujisikia vizuri.
3. Kupumzika na kustareheka.
4. Kuondoa uchofu au maumivu.
5. Dini na imani.
6. Kupata au kuokoa fedha zaidi.
7. Kupata matokeo ya tofauti.
8. Kulipa kisasi.
9. Mapenzi.
10. Nguvu na mamlaka.
Chochote unachouza au kuwashawishi wengine, gusa moja au zaidi kwenye hisia hizo na utakuwa na ushawishi zaidi.
Kocha.