
Sehemu ya tatu ya msingi wa mafanikio tunaouishi kila siku ni kujituma.
Kujituma ni kuweka juhudi na umakini mkubwa kwenye kile unachofanya ili uweze kupata matokeo yaliyo bora.
Ni kwenda hatua ya ziada kwa kufanya zaidi ya watu wanavyotegemea ufanye au wanavyokulipa. Ni kuzalisha thamani iliyo kubwa sana.
Kwa kuwa unajua asili haipendi kudaiwa, hulipa kulingana na thamani inayozalishwa, hivyo unapojituma, lazima ufanikiwe kwenye chochote unachofanya.
Usifanye kwa mazoea, bali fanya kwa ubora zaidi na dunia itakulipa kulingana na kiwango unachofanya.
Ukurasa wa kusoma ni njia 6 za kuongeza ushawishi, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/03/24/2275
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma