
Jinsi watu wanavyokuchukulia, ni wewe mwenyewe umewafundisha. Wanaiga kile unachojifanyia mwenyewe na ndiyo wanakufanyia.
Kama unajiheshimu, watu lazima wakuheshimu, ukijidharau wanakudharau. Kama unajithamini na watu pia watalazimika kukuthamini.
Ndiyo maana ni muhimu sana kujiwekea viwango vyako vya kimaisha na kuviishi, maana bila hivyo watu watakuwekea viwango vya chini ili wakutumie watakavyo wao.
Kama kuna namna watu wanakuchukulia na hupendi, usihangaike nao, anza kujichukulia wewe tofauti na wao wataiga hilo.
Ukurasa wa kusoma ni jua kukuangaza bure; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/04/04/2286
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma
Asante Sana kocha kwa tafakari, nakushkru sana,hakuna haja ya kuangaika na watu,angaika wewe mwenyewe kujitengeneza tabia na mwonekano wako.
LikeLike
Karibu Beatus
LikeLike