2288; Watoze watu wakikukatisha kwenye hiki…

Joe Girard, aliyekuwa muuzaji mkubwa wa magari amewahi kusema kitu anachopenda zaidi ni kulala, hivyo kama mtu anakatisha usingizi wake, lazima awatoze.
Kuna kitu kikubwa sana cha kujifunza hapa, kuhusu kuweka vipaumbele kwenye maisha yako.
Tumeshajifunza umuhimu wa kufanya kile unachopenda na kuangalia namna wengine wanaweza kukulipa kwa kufanya hicho.
Kitu muhimu zaidi hapa ni kuweza kuwatoza zaidi wale wanaokutoa kwenye kile unachopenda kufanya, kama siyo kinachokuingizia fedha.
Kwa vyovyote vile, wafanye watu wawe tayari kuthamini chochote wanachotaka ufanye na siyo tu kukutaka uwafanyie bure.
Kocha.