
Majuto ni kitu kisichokwepeka kwenye maisha yako.
Kwa kila jambo utakalofanya, kuna majuto utakuwa nayo.
Hasa pale unapokuwa na machaguo mbalimbali na inabidi uchague moja, haijalishi utachagua lililo bora kiasi gani, kuna wakati utaona bora ungechagua kingine.
Hivyo usiangalie kutokuwa na majuto kabisa, bali angalia maamuzi ambayo yatakupa majuto madogo na yasiyodumu muda mrefu.
Lakini pia kila unapokuwa na majuto, jikumbushe hata ungefanya hayo maamuzi mengine unayotamani ungefanya, bado kuna majuto ungekuwa nayo.
Usikubali majuto yawe kitu kinachokurudisha nyuma au kukuzuia kuyafurahia maisha yako.
Ukurasa wa kusoma ni katili isiyo katili; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/04/05/2287
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma