Watu wanaotaka mafanikio kwa njia za mkato, huwa wanakimbilia kutumia kiki.

Kufanya mambo ya kijinga ambayo yanawapa umaarufu wa haraka, lakini usio na heshima.

Umaarufu wa aina hiyo huwa haudumu muda mrefu na huacha madhara makubwa.

Wewe jenga mafanikio na umaarufu wako kupitia heshima na heshima inajengwa kupitia kutoa thamani kubwa kwa wengine.

Njia ya heshima ni ndefu na ya muda mrefu, lakini matokeo yake yanadumu kuliko ya kiki za muda mfupi.

Utaona wengi wakihangaika na kiki, wewe hangaika na heshima.

Ukurasa wa kusoma ni kutoomba ulichozaliwa nacho, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/04/07/2289

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma