
Watu wengi wanakwama kwenye maisha kwa sababu wanataka kupata kwanza kabla hawajatoa.
Mtu anataka kazi imlipe vizuri ndiyo aweke juhudi au biashara impe faida kubwa ndiyo aweke umakini wake mkubwa. Kinachotokea ni hawapati kile wanachotaka.
Ili kupata unachotaka, anza kutoa kwanza. Anza kuweka juhudi kubwa kwenye kazi na biashara yako na baadaye kipato chako kitaongezeka. Toa thamani kubwa kwa wengine na watakuwa tayari kukupa unachotaka.
Kama kuna kitu unakitafuta sana na hukipati, hebu anza kujiuliza ni nini umetoa ili kupata unachotaka. Utagundua hujatoa kwa usahihi, hivyo kwa kuanzia hapo, unaweza kupata unachotaka.
Ukurasa wa kusoma ni kuendelea kukaa kimya kama ulichagua hivyo; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/04/08/2290
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma