Pale maisha yako yalipo sasa ni matokeo ya maamuzi ambayo umefanya siku za nyuma.

Hata kutokufanya maamuzi ni sehemu ya maamuzi, kwa sababu unakuwa umeruhusu wengine ndiyo wakufanyie maamuzi.

Na ukifanya maamuzi halafu usichukue hatua nayo pia ni maamuzi umefanya kutokuchukua hatua na yamekufikisha ulipo sasa.

Njia pekee ya kuyabadili maisha yako ni kubadili maamuzi unayofanya na maamuzi juu ya maamuzi.

Kama umekuwa unaamua kitu halafu wakati wa kufanya ukifika unaamua kutokukifanya, badilika na ukishaanua, amua pia kufanya kama ulivyoamua.

Ni maamuzi yetu ndipo nguvu kubwa ya mabadiliko kwetu ilipo, tufanye maamuzi mzuri na kuyafanyia kazi.

Ukurasa wa kusoma ni ukishafanya maamuzi; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/04/30/2312

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma