Njia ya uhakika ya kuikosa furaha ni kuweka malengo ya kupata furaha kupitia yale unayofanya.

Utapambana kuyafanya lakini hutapata furaha au ukipata itakuwa ya muda mfupi tu.

Furaha haitafutwi au kukimbiliwa, bali furaha huwa inavutiwa na namna mtu anayaishi maisha yake na kufanya mambo yake.

Unapojisalimisha kufanya kitu kikubwa kuliko wewe na kukifanya kwa ubora ambao utawanufaisha wengine, furaha inakuwa ni matokeo.

Hujalenga furaha lakini unapata kwa sababu kwa kufanya kilicho kikubwa, unatumia kile kilicho ndani yako na unakuwa umeyaishi maisha yako.

Furaha ni matokeo ya wewe kuyaishi maisha yako na siyo kukimbizana na yale unayoona yatakupa furaha.

Ukurasa wa kusoma leo ni kukimbiza kipepeo; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/05/05/2317

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma