Huwa kuna kichekesho cha mtu alienda kuchota maji kisimani akakuta kuna watu wengi. Akatafuta mbinu ya kuwadanganya ili waondoke na aweze kuchota maji.

Hivyo akawaambia mbona nyie mko hapa wakati kuna gari linatoa zawadi nzuri liko kule? Watu hao wakamuuliza unasema kweli? Akajibu ni kweli kabisa, wengine wanajipatia zawadi na nyie mnapitwa. Kusikia hivyo watu hao wakaondoka wote kukimbilia walipoambiwa kuna zawadi.

Yule mtu akabaki kisimani peke yake, badala ya kuchota maji ambalo lilikuwa lengo lake, akajiuliza mbona wameamini wote na kwenda? Labda kuna zawadi kweli, basi na yeye akatoka kuongozana nao kwenda kupata zawadi 😂.

Ni kichekesho ila kina ujumbe mkubwa sana, kile unachowashauri wengine ndiyo unakuwa umejishauri na wewe mwenyewe pia. Hivyo kuwa makini mno na ushauri unaotoa kwa wengine.

Kujua athari tatu za ushauri unaotoa kwa wengine fungua hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/05/08/2320

#NUK #AUH #KUH