Hekima na upumbavu ni vile vile tangu enzi na enzi, hakuna kipya kwenye hayo. Mabadiliko yapo kwa namna vinatumika kwenye enzi husika.

Wenye hekima wamekuwa wanafanya mambo yale yale huku wapumbavu pia wakifanya yale yale. Huna haja ya kuja na hekima au upumbavu mpya, angalia tu namna wengine wamekuwa wanaishi maisha yao.

Ukijiangalia na wewe pia, utajikuta unarudia hayo hayo. Unachagua kuishi hekima au kuishi upumbavu hivyo usilalamikie matokeo unayopata, angalia maisha uliyochagua kuyaishi.

Ukurasa wa kusoma ni kuhusu hekima na upumbavu mpya; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/05/10/2322

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma