2324; Maarifa Na Hekima…
Huwezi kuwa na hekima bila ya kuwa na maarifa, lakini unaweza kuwa na maarifa usiwe na hekima.
Maarifa ni kujua vitu vingi, hekima ni kujua jinsi ya kutumia maarifa hayo.
Maarifa unayapata, ila hekima unaishi.
Maarifa yanakusanywa, ila hekima inanolewa.
Unaweza kuyapoteza maarifa lakini hekima inadumu milele.
Unaweza kujisifia una maarifa mengi, ila hekima ni kile watu wanachoona kwako.
Unajijengea hekima kwa kuyaishi maarifa unayoyapata.
Na yakishakuwa sehemu ya maisha yako, yanakuwa wewe na huwezi kuyapoteza.
Kila maarifa unayopata, yageuze kuwa hekima ili maisha yako yaweze kuwa bora zaidi.
Kocha.