
Unaweza ukawaambia watu kwamba umesoma vitabu vingi au unajua mambo mengi sana. Lakini huwezi kuwaambia watu kwamba una hekima kubwa.
Hekima ni kitu ambacho watu wanakiona kwako, kutokana na jinsi unavyoyatumia maarifa ambayo umeyapata.
Hivyo pata maarifa mengi uwezavyo, ila yatumie kujijengea hekima, kwa kuyaweka kwenye matendo yale uliyojifunza.
Hakuna asiyejua kama unataka kufikia utajiri mapato yanapaswa kuwa makubwa kuliko matumizi. Lakini wengi matumizi yao ni makubwa kuliko mapato, siyo kwa sababu hawana maarifa, ila kwa sababu hawana hekima inapokuja kwenye swala la fedha.
Maarifa unayopata hayatakuwa na maana kwako kama hutayatumia kujijengea hekima.
Ukurasa wa kusoma ni tofauti ya maarifa na hekima; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/05/12/2324
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma